Yoeli 1:3 - Swahili Revised Union Version Waambieni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wasimulieni watoto wenu jambo hili, nao wawasimulie watoto wao, na watoto wao wakisimulie kizazi kifuatacho. Biblia Habari Njema - BHND Wasimulieni watoto wenu jambo hili, nao wawasimulie watoto wao, na watoto wao wakisimulie kizazi kifuatacho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wasimulieni watoto wenu jambo hili, nao wawasimulie watoto wao, na watoto wao wakisimulie kizazi kifuatacho. Neno: Bibilia Takatifu Waelezeni watoto wenu, na watoto wenu wawaambie watoto wao, na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata. Neno: Maandiko Matakatifu Waelezeni watoto wenu, na watoto wenu wawaambie watoto wao, na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata. BIBLIA KISWAHILI Waambieni watoto wenu habari yake, Watoto wenu wakawaambie watoto wao, Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine. |
Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;
Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.
nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.