Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
Yoeli 1:20 - Swahili Revised Union Version Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe; Kwa maana vijito vya maji vimekauka, Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata wanyama wa porini wanakulilia wewe, maana, vijito vya maji vimekauka, moto umemaliza malisho nyikani. Biblia Habari Njema - BHND Hata wanyama wa porini wanakulilia wewe, maana, vijito vya maji vimekauka, moto umemaliza malisho nyikani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata wanyama wa porini wanakulilia wewe, maana, vijito vya maji vimekauka, moto umemaliza malisho nyikani. Neno: Bibilia Takatifu Hata wanyama pori wanakuonea shauku; vijito vya maji vimekauka, na moto umeteketeza malisho yote ya mbugani. Neno: Maandiko Matakatifu Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku; vijito vya maji vimekauka, na moto umeteketeza malisho yote ya mbugani. BIBLIA KISWAHILI Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe; Kwa maana vijito vya maji vimekauka, Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani. |
Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.
Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?
Kwa sababu ya nchi iliyopasuka, Kwa kuwa mvua haikunyesha katika nchi, Wakulima wametahayarika, Na kuvifunika vichwa vyao.
Manabii walionitangulia, na waliokutangulia, walitabiri habari za vita, na za mabaya na za tauni juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa.
Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika.