Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Yakobo 2:12 - Swahili Revised Union Version Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. Biblia Habari Njema - BHND Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru. BIBLIA KISWAHILI Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. |
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.