Yakobo 1:3 - Swahili Revised Union Version mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Biblia Habari Njema - BHND kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. Neno: Bibilia Takatifu kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Neno: Maandiko Matakatifu kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. BIBLIA KISWAHILI mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. |
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.
wale ambao kwa subira katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoharibika, watapewa uzima wa milele;
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu subira, na katika subira yenu utauwa,