Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Walawi 9:5 - Swahili Revised Union Version

Nao wakayaleta hayo yaliyoagizwa na Musa wakayaweka mbele ya hema ya kukutania; kisha mkutano wote ukakaribia wakasimama mbele za BWANA.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Waisraeli wakaleta vyote hivyo mbele ya hema la mkutano kama Mose alivyowaamuru na jumuiya yote ikaenda kusimama mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Waisraeli wakaleta vyote hivyo mbele ya hema la mkutano kama Mose alivyowaamuru na jumuiya yote ikaenda kusimama mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Waisraeli wakaleta vyote hivyo mbele ya hema la mkutano kama Mose alivyowaamuru na jumuiya yote ikaenda kusimama mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Wakavileta vile vitu Musa alivyowaagiza mbele ya Hema la Kukutania, na kusanyiko lote wakakaribia na kusimama mbele za Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Wakavileta vile vitu Musa alivyowaagiza mbele ya Hema la Kukutania, nalo kusanyiko lote likakaribia na kusimama mbele za bwana.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nao wakayaleta hayo yaliyoagizwa na Musa wakayaweka mbele ya hema ya kukutania; kisha mkutano wote ukakaribia wakasimama mbele za BWANA.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Walawi 9:5
7 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu, ili kulipandisha sanduku la BWANA, mpaka mahali pake alipoliwekea tayari.

Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha Torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli.

Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima.

na ng'ombe dume, na kondoo dume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za BWANA; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, BWANA hivi leo atawatokea.

Kisha Musa akasema, Neno aliloliagiza BWANA kwamba mlifanye ni hili; na huo utukufu wa BWANA utawatokea.

Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii;