Walawi 13:44 - Swahili Revised Union Version yeye ni mtu mwenye ukoma, ni najisi; na kuhani hana budi atasema kuwa ni najisi; pigo lake liko katika kichwa chake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema basi, mtu huyo ana ukoma; yeye ni najisi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ugonjwa wake upo kwenye kichwa chake. Biblia Habari Njema - BHND basi, mtu huyo ana ukoma; yeye ni najisi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ugonjwa wake upo kwenye kichwa chake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza basi, mtu huyo ana ukoma; yeye ni najisi. Kuhani atamtangaza mtu huyo kuwa najisi. Ugonjwa wake upo kwenye kichwa chake. Neno: Bibilia Takatifu mtu huyo ni mgonjwa, na ni najisi. Kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya kidonda kwenye kichwa chake. Neno: Maandiko Matakatifu mtu huyo ni mgonjwa, na ni najisi. Kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya kidonda kwenye kichwa chake. BIBLIA KISWAHILI yeye ni mtu mwenye ukoma, ni najisi; na kuhani hana budi atasema kuwa ni najisi; pigo lake liko katika kichwa chake. |
Mbona mnataka kupigwa, hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.
Ndipo kuhani atamwangalia; kivimbe cha pigo kikiwa cheupe na chekundu chekundu, katika kichwa chake chenye upara, au katika kipaji chake cha upara, kama vile kuonekana kwa ukoma katika ngozi ya mwili;
Mtu mwenye ukoma aliye na pigo ndani yake, atavaa nguo zilizoraruka, na nywele timutimu; na ataufunika mdomo wake wa juu na kusema, “Ni najisi, ni najisi”.
Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!