Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako.
Wafilipi 4:14 - Swahili Revised Union Version Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. Neno: Bibilia Takatifu Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini, mlifanya vyema kushiriki nami katika taabu zangu. BIBLIA KISWAHILI Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. |
Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako.
Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako;
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumia kwa mambo yao ya mwili.
vile vile kama ilivyo wajibu wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kutetea Injili na kuithibitisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.
Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
Waamuru watende mema, wawe matajiri katika kutenda mema, wawe wakarimu na wawe tayari kushiriki na wengine;
pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo.
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.