usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Wafilipi 4:13 - Swahili Revised Union Version Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. BIBLIA KISWAHILI Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. |
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Mmoja ataniambia, Kwa BWANA, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika.
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;