Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai.
Wafilipi 2:4 - Swahili Revised Union Version Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake. Biblia Habari Njema - BHND Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake. Neno: Bibilia Takatifu Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine. Neno: Maandiko Matakatifu Kila mmoja wenu asiangalie faida yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine. BIBLIA KISWAHILI Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. |
Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai.
Musa akawaambia wana wa Gadi na wana wa Reubeni, Je! Ndugu zenu waende vitani nanyi mtaketi hapa?
bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.
Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.