Waebrania 7:12 - Swahili Revised Union Version Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana ukuhani ukibadilika, ni lazima sheria nayo ibadilike. Biblia Habari Njema - BHND Maana ukuhani ukibadilika, ni lazima sheria nayo ibadilike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana ukuhani ukibadilika, ni lazima sheria nayo ibadilike. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa ukuhani ukibadilika, lazima sheria nayo ibadilike. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa yanapotokea mabadiliko ya ukuhani, pia lazima yawepo mabadiliko ya sheria. BIBLIA KISWAHILI Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike. |
Hapo ndipo utakapozikumbuka njia zako, na kutahayarika, hapo utakapowakaribisha dada zako, walio wakubwa wako na wadogo wako; nami nitakupa hao wawe binti zako, lakini si kwa agano lako.
Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine awepo, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?
Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hilo aliyeihudumia madhabahu.
kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kunawa kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.