Waebrania 6:5 - Swahili Revised Union Version na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za wakati ujao, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema na kuonja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, Biblia Habari Njema - BHND na kuonja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza na kuonja wema wa neno la Mungu na nguvu za ulimwengu ujao, Neno: Bibilia Takatifu ambao wameonja uzuri wa neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, Neno: Maandiko Matakatifu ambao wameonja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, BIBLIA KISWAHILI na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za wakati ujao, |
Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.
Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema,
Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.