Waebrania 6:14 - Swahili Revised Union Version akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” Biblia Habari Njema - BHND Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu alisema: “Hakika nitakubariki na nitakupa wazawa wengi.” Neno: Bibilia Takatifu akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” Neno: Maandiko Matakatifu akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” BIBLIA KISWAHILI akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. |
akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;
akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele.
Watoto wao nao uliwaongeza kama nyota za mbinguni, ukawaingiza katika nchi ile, uliyowaambia baba zao kuwa wataingia kuimiliki.
Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.
Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Abrahamu kwa njia ya ahadi.
BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi.
Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.
watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.