Waebrania 3:19 - Swahili Revised Union Version Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini. Biblia Habari Njema - BHND Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. BIBLIA KISWAHILI Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao. |
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Na hao pia, wasipokaa katika kutoamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.
ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.
Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.