Waebrania 10:6 - Swahili Revised Union Version Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi. Biblia Habari Njema - BHND Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi. Neno: Bibilia Takatifu sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukupendezwa nazo. Neno: Maandiko Matakatifu sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukupendezwa nazo. BIBLIA KISWAHILI Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; |
Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Umetuzidishia ila masikio, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.
na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
mkaende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
Naye Samweli akasema, Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.