Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Waebrania 10:37 - Swahili Revised Union Version

Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maana kama yasemavyo Maandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maana kama yasemavyo Maandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maana kama yasemavyo Maandiko: “Bado kidogo tu, na yule anayekuja, atakuja, wala hatakawia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa kuwa, “Bado kitambo kidogo tu, yeye ajaye atakuja wala hatakawia.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu, “Yeye ajaye atakuja wala hatakawia.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Waebrania 10:37
11 Marejeleo ya Msalaba  

Njooni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.


Aliye mdogo zaidi atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, BWANA, nitayahimiza hayo wakati wake.


Wewe ndiwe yule ajaye, au tumngojee mwingine?


Nawaambia, atawapatia haki upesi; lakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?


Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yuko karibu.


wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.


Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.


Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.


Yeye ayashuhudiaye haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.