Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Ufunuo 9:8 - Swahili Revised Union Version Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Biblia Habari Njema - BHND Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Neno: Bibilia Takatifu Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. Neno: Maandiko Matakatifu Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. BIBLIA KISWAHILI Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. |
Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu, Lenye nguvu, tena halina hesabu; Meno yake ni kama meno ya simba, Naye ana magego ya simba mkubwa.
Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora.
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;