akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vile vile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Ruthu 1:21 - Swahili Revised Union Version Mimi nilitoka nikiwa nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.” Biblia Habari Njema - BHND Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilipoondoka hapa, nilikuwa na vitu vingi, lakini sasa Mwenyezi-Mungu amenirudisha mikono mitupu. Mbona mwaniita Naomi na hali Mwenyezi-Mungu ameniadhibu, naye Mungu Mwenye Nguvu amenitesa.” Neno: Bibilia Takatifu Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Mwenyezi Mungu amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Mwenyezi Mungu amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.” Neno: Maandiko Matakatifu Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini bwana amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? bwana amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.” BIBLIA KISWAHILI Mimi nilitoka nikiwa nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? |
akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vile vile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Wewe unafanya upya ushahidi wako juu yangu, Na kuongeza kisirani chako juu yangu; Ukileta jeshi baada ya jeshi juu yangu.
Umenishika sana, na kuwa ushahidi juu yangu; Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami sitasita kutoa ushahidi juu ya wachawi; na juu ya wazinzi, na juu ya waapao kwa uongo; juu ya wamwoneao mwajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.
je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umetoka juu yangu.