Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.
Obadia 1:16 - Swahili Revised Union Version Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kuyumbayumba, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana, kama walivyokunywa kikombe cha ghadhabu yangu kwenye mlima wangu mtakatifu ndivyo na mataifa jirani yatakavyokunywa; watakunywa na kupepesuka, wataangamia kana kwamba hawakuwahi kuwapo duniani. Biblia Habari Njema - BHND Maana, kama walivyokunywa kikombe cha ghadhabu yangu kwenye mlima wangu mtakatifu ndivyo na mataifa jirani yatakavyokunywa; watakunywa na kupepesuka, wataangamia kana kwamba hawakuwahi kuwapo duniani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana, kama walivyokunywa kikombe cha ghadhabu yangu kwenye mlima wangu mtakatifu ndivyo na mataifa jirani yatakavyokunywa; watakunywa na kupepesuka, wataangamia kana kwamba hawakuwahi kuwapo duniani. Neno: Bibilia Takatifu Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo; watakunywa na kunywa, nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo, watakunywa na kunywa, nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kuyumbayumba, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe. |
Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.
Maana BWANA asema hivi, Tazama, wale wasioandaliwa kunywea kikombe, watakinywea, ni hakika; na wewe je! U mtu ambaye hataadhibiwa kabisa? Hukosi utaadhibiwa, naam, kunywa utakunywa.
Furahi, ushangilie, Ee binti Edomu, Ukaaye katika nchi ya Usi; Hata kwako kikombe kitapita, Utalewa, na kujifanya uchi.
Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
Wanakuja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga.
Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje?