Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
Nehemia 9:21 - Swahili Revised Union Version Naam, muda wa miaka arubaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala miguu yao haikuvimba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukawatunza jangwani kwa miaka arubaini na hawakukosa chochote; mavazi yao hayakuchakaa wala nyayo zao hazikuvimba. Biblia Habari Njema - BHND Ukawatunza jangwani kwa miaka arubaini na hawakukosa chochote; mavazi yao hayakuchakaa wala nyayo zao hazikuvimba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukawatunza jangwani kwa miaka arubaini na hawakukosa chochote; mavazi yao hayakuchakaa wala nyayo zao hazikuvimba. Neno: Bibilia Takatifu Kwa miaka arobaini uliwatunza jangwani. Hawakukosa chochote, na nguo zao hazikuchakaa wala miguu yao haikuvimba. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa miaka arobaini uliwatunza jangwani. Hawakukosa chochote, na nguo zao hazikuchakaa wala miguu yao haikuvimba. BIBLIA KISWAHILI Naam, muda wa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala miguu yao haikuvimba. |
Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arubaini, hata walipofikia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikia mipakani mwa nchi ya Kanaani.
Je! Mliniletea dhabihu na sadaka jangwani muda wa miaka arubaini, enyi nyumba ya Israeli?
Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubariki katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arubaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.
Nami miaka arubaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.
Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.