Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Nehemia 5:6 - Swahili Revised Union Version Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Niliposikia malalamiko yao, nilikasirika sana. Biblia Habari Njema - BHND Niliposikia malalamiko yao, nilikasirika sana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Niliposikia malalamiko yao, nilikasirika sana. Neno: Bibilia Takatifu Niliposikia kilio chao na malalamiko haya, nilikasirika sana. Neno: Maandiko Matakatifu Niliposikia kilio chao na malalamiko haya, nilikasirika sana. BIBLIA KISWAHILI Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo. |
Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.
Nami nikasikitika sana; basi nikavitupa nje vyombo vyote vya Tobia vitoke humo chumbani.
Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na maofisa, nikawaambia, Nyote mnatoza watu riba, mtu na ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kukabiliana nao.
Tena hao watumishi wako wote wataniteremkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.
Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao.
Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.