Akasema, Washami wakiwa ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe.
Nehemia 4:20 - Swahili Revised Union Version basi mahali popote mtakaposikia sauti ya baragumu, kimbilieni kwetu; Mungu wetu atatupigania. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukiwa mahali popote unapofanya kazi, mara utakaposikia tarumbeta, kimbilia kwetu. Mungu wetu atatupigania.” Biblia Habari Njema - BHND Ukiwa mahali popote unapofanya kazi, mara utakaposikia tarumbeta, kimbilia kwetu. Mungu wetu atatupigania.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukiwa mahali popote unapofanya kazi, mara utakaposikia tarumbeta, kimbilia kwetu. Mungu wetu atatupigania.” Neno: Bibilia Takatifu Popote mtakaposikia sauti ya baragumu, jiungeni nasi huko. Mungu wetu atatupigania!” Neno: Maandiko Matakatifu Popote mtakaposikia sauti ya baragumu, jiungeni nasi huko. Mungu wetu atatupigania!” BIBLIA KISWAHILI basi mahali popote mtakaposikia sauti ya baragumu, kimbilieni kwetu; Mungu wetu atatupigania. |
Akasema, Washami wakiwa ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe.
Nikawaambia wakuu, maofisa na watu wengine; Kazi hii ni nyingi, tena kubwa, nasi tumetawanyika juu ya ukuta, kila mtu akiwa mbali na mwenzake;
Hivyo tukajitia katika kazi hiyo; na nusu yao waliishika mikuki, tangu alfajiri hadi nyota zikatokea.
Akayakwamisha magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa shida; na Wamisri wakasema, Na tuwakimbieni Waisraeli; kwa kuwa BWANA anawapigania.
Hapo ndipo atakapotokea BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama anavyopigana siku ya vita.
BWANA, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu;
kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.