Na baada yao akajenga Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akajenga Hatushi, mwana wa Hashabneya.
Nehemia 3:9 - Swahili Revised Union Version Na baada yao Refaya, mwana wa Huri akajenga, mtawala wa nusu ya Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sehemu inayofuata ilijengwa upya na Refaya, mwana wa Huri, mkuu wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Sehemu inayofuata ilijengwa upya na Refaya, mwana wa Huri, mkuu wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sehemu inayofuata ilijengwa upya na Refaya, mwana wa Huri, mkuu wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Refaya mwana wa Huri, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia. Neno: Maandiko Matakatifu Refaya mwana wa Huri, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia. BIBLIA KISWAHILI Na baada yao Refaya, mwana wa Huri akajenga, mtawala wa nusu ya Yerusalemu. |
Na baada yao akajenga Yedaya, mwana wa Harumafu, kuielekea nyumba yake. Na baada yake akajenga Hatushi, mwana wa Hashabneya.
Na baada yake akajenga Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya sehemu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.
Baada yake akajenga Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya wapiganaji.
Baada yake wakajenga Walawi, Rehumu, mwana wa Bani. Baada yake akajenga Hashabia, mkuu wa nusu ya mtaa wa Keila, kwa mtaa wake.