Tena Uzia akaujengea Yerusalemu minara, penye Lango la Pembeni, na penye Lango la Bondeni, na ugeukapo ukuta, akaitia nguvu.
Nehemia 3:19 - Swahili Revised Union Version Na baada yake Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mispa, akajenga sehemu nyingine, inayoelekeana na njia ya kupanda kwa ghala ya silaha, pembeni mwa ukuta. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sehemu inayofuata inayoelekeana na ghala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ilijengwa upya na Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mizpa. Biblia Habari Njema - BHND Sehemu inayofuata inayoelekeana na ghala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ilijengwa upya na Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mizpa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sehemu inayofuata inayoelekeana na ghala ya silaha kwenye pembe ya ukuta ilijengwa upya na Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mizpa. Neno: Bibilia Takatifu Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, hadi kwenye pembe ya ukuta. Neno: Maandiko Matakatifu Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta. BIBLIA KISWAHILI Na baada yake Ezeri, mwana wa Yeshua, mkuu wa Mispa, akajenga sehemu nyingine, inayoelekeana na njia ya kupanda kwa ghala ya silaha, pembeni mwa ukuta. |
Tena Uzia akaujengea Yerusalemu minara, penye Lango la Pembeni, na penye Lango la Bondeni, na ugeukapo ukuta, akaitia nguvu.
Tena Walawi; Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa juu ya shukrani, yeye na ndugu zake.
Na lango la chemchemi akalijenga Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa Mispa akalitengeneza lango la Chemchemi akalijenga na kulifunika, akasimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.
Baada yake wakajenga ndugu zao, Binui, mwana wa Henadadi, mkuu wa nusu ya mtaa wa Keila.
Baada yake Binui, mwana wa Henadadi, alitengeneza sehemu nyingine, kuanzia kwenye nyumba ya Azaria mpaka ugeukapo ukuu, na mpaka pembeni.