Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Nehemia 10:39 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa Israeli na Walawi watayapeleka matoleo ya nafaka, divai na mafuta ya zeituni kwenye vyumba ambamo vyombo vya patakatifu vinatunzwa na ambamo makuhani, wangoja malango na waimbaji wana vyumba vyao. Na daima tutaijali nyumba ya Mungu wetu. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa Israeli na Walawi watayapeleka matoleo ya nafaka, divai na mafuta ya zeituni kwenye vyumba ambamo vyombo vya patakatifu vinatunzwa na ambamo makuhani, wangoja malango na waimbaji wana vyumba vyao. Na daima tutaijali nyumba ya Mungu wetu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa Israeli na Walawi watayapeleka matoleo ya nafaka, divai na mafuta ya zeituni kwenye vyumba ambamo vyombo vya patakatifu vinatunzwa na ambamo makuhani, wangoja malango na waimbaji wana vyumba vyao. Na daima tutaijali nyumba ya Mungu wetu. Neno: Bibilia Takatifu Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji. “Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji. “Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.” BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu. |
Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; Konania, Mlawi aliwekwa kuwa mkuu na Shimei nduguye akawa masaidizi wake.
Na Israeli wote, siku za Zerubabeli, na siku za Nehemia, walitoa sehemu za waimbaji na mabawabu, kama ilivyohusika kila siku; nao wakawatakasia Walawi; na Walawi wakawatakasia wana wa Haruni.
Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.
Kwa ajili ya hayo utawaambia, Mtakapoinua humo hayo yaliyo mema, ndipo yatahesabiwa kuwa ya Walawi, kama mavuno ya sakafu ya kupuria nafaka, na kama mavuno ya kinu cha kusindikia zabibu.
Usile ndani ya makazi yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zozote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.