BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
Mwanzo 8:16 - Swahili Revised Union Version Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Toka katika safina, wewe pamoja na mkeo, wanao na wake zao. Biblia Habari Njema - BHND “Toka katika safina, wewe pamoja na mkeo, wanao na wake zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Toka katika safina, wewe pamoja na mkeo, wanao na wake zao. Neno: Bibilia Takatifu “Toka katika safina, wewe na mkeo, na wanao na wake zao. Neno: Maandiko Matakatifu “Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. BIBLIA KISWAHILI Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. |
BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye;
Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika.
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.
Na hao makuhani waliolichukua sanduku la Agano la BWANA wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hadi taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.
Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hadi mambo yote BWANA aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka.