Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Mwanzo 49:16 - Swahili Revised Union Version Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake, kama mojawapo ya makabila ya Israeli. Biblia Habari Njema - BHND “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake, kama mojawapo ya makabila ya Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake, kama mojawapo ya makabila ya Israeli. Neno: Bibilia Takatifu “Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu “Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli. BIBLIA KISWAHILI Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; |
Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Na apandaye akaanguka chali.
Kisha beramu ya kambi ya wana wa Dani, ambayo ilikuwa ni nyuma ya makambi yote, ikasafiri, kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.