Mwanzo 4:22 - Swahili Revised Union Version Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. Biblia Habari Njema - BHND Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. Neno: Bibilia Takatifu Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini, ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. Neno: Maandiko Matakatifu Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. BIBLIA KISWAHILI Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama. |
Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni ninachosema; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
Unitumie mtu stadi wa kuchonga dhahabu, fedha, shaba na chuma, na wa nguo za urujuani, nyekundu na samawati, ajuaye kutia nakshi, awe mmoja wa mastadi walioko pamoja nami Yuda na Yerusalemu ambao aliwaweka baba yangu Daudi.
Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake mnaweza kuchimba shamba.