Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Mwanzo 30:7 - Swahili Revised Union Version Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena na kumzalia Yakobo mtoto wa pili wa kiume. Biblia Habari Njema - BHND Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena na kumzalia Yakobo mtoto wa pili wa kiume. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena na kumzalia Yakobo mtoto wa pili wa kiume. Neno: Bibilia Takatifu Bilha mjakazi wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Neno: Maandiko Matakatifu Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. BIBLIA KISWAHILI Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. |
Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Hao ndio wana wa Bilha, ambaye Labani alimpa Raheli, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao; wote walikuwa watu saba.
Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Naftali, fungu moja.
Katika wana wa Naftali, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;