Mwanzo 3:21 - Swahili Revised Union Version BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Neno: Bibilia Takatifu Bwana Mwenyezi Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Neno: Maandiko Matakatifu bwana Mwenyezi Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. BIBLIA KISWAHILI BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. |
BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajitambua kuwa wako uchi, wakashona majani ya mtini, na kujifanyia mavazi ya kusitiri uchi wao.
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile tunavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.
Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.