Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.
Mwanzo 26:30 - Swahili Revised Union Version Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Isaka akawafanyia karamu, nao wakala na kunywa. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Isaka akawafanyia karamu, nao wakala na kunywa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Isaka akawafanyia karamu, nao wakala na kunywa. Neno: Bibilia Takatifu Basi Isaka akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Isaka akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. BIBLIA KISWAHILI Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa. |
Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.
Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.
Yakobo akachinja sadaka katika mlima, akawaita ndugu zake waje wale chakula, nao wakala chakula, wakakaa usiku kucha mlimani.
Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu.
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;