Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini.
Mwanzo 12:9 - Swahili Revised Union Version Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha Abramu akaendelea kusafiri kuelekea upande wa Negebu. Biblia Habari Njema - BHND Kisha Abramu akaendelea kusafiri kuelekea upande wa Negebu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha Abramu akaendelea kusafiri kuelekea upande wa Negebu. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu. BIBLIA KISWAHILI Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini. |
Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini.
Akaendelea kusafiri kutoka kusini mpaka Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza, kati ya Betheli na Ai;
Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.
Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni kaka yangu.
Basi Isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana alikaa katika nchi ya kusini.
Ufunuo juu ya wanyama wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba angurumaye, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.
Musa akawatuma ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,
geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati.