Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Mwanzo 10:4 - Swahili Revised Union Version Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu. Biblia Habari Njema - BHND Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu. Neno: Bibilia Takatifu Wana wa Yavani walikuwa: Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Neno: Maandiko Matakatifu Wana wa Yavani walikuwa: Al-Yasa, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. BIBLIA KISWAHILI Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. |
Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
Ufunuo juu ya Tiro. Toeni sauti za uchungu, enyi merikebu za Tarshishi, kwa maana umeharibika kabisa, hata hapana nyumba, hapana mahali pa kuingia; toka nchi ya Kitimu wamefunuliwa habari.
Naye akasema, Usizidi kufurahi, ewe bikira uliyeaibishwa, binti wa Sidoni, haya, ondoka, uende hadi Kitimu; huko nako hutapata raha.
Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa.
Merikebu za Tarshishi zilikuwa misafara yako, kwa bidhaa yako; nawe ulijazwa sana, ukawa mtukufu sana, katika moyo wa bahari.
kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.
Tanga lako lilikuwa la kitani safi itokayo Misri, iliyotiwa taraza, ili iwe bendera kwako; na chandarua chako kilikuwa cha rangi ya samawati na urujuani toka visiwa vya Elisha.
Maana merikebu za Kitimu zitakuja kupigana naye; basi atavunjika moyo, naye atarudi na kulighadhibikia hilo agano takatifu; na kutenda kadiri apendavyo; naam, atarudi, na kuwasikiliza walioacha hilo agano takatifu.
Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu, Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha, Yeye naye atapata uharibifu.