kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mhubiri 3:10 - Swahili Revised Union Version Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi nimeiona kazi ambayo binadamu amepewa na Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Mimi nimeiona kazi ambayo binadamu amepewa na Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi nimeiona kazi ambayo binadamu amepewa na Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu. Neno: Maandiko Matakatifu Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu. BIBLIA KISWAHILI Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. |
kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu.
wala hatukula chakula kwa mtu yeyote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulifanya kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.