Methali 8:11 - Swahili Revised Union Version Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari; chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami. Biblia Habari Njema - BHND “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari; chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mimi Hekima nina thamani kuliko johari; chochote unachotamani hakiwezi kulingana nami. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye. BIBLIA KISWAHILI Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo. |
Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Wala si ng'ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya?