Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Methali 7:10 - Swahili Revised Union Version Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Punde kijana akakutana na huyo mwanamke; amevalia kama malaya, ana mipango yake. Biblia Habari Njema - BHND Punde kijana akakutana na huyo mwanamke; amevalia kama malaya, ana mipango yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Punde kijana akakutana na huyo mwanamke; amevalia kama malaya, ana mipango yake. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya hila. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu. BIBLIA KISWAHILI Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; |
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?
Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Twaa kinubi, tembea mjini, Ewe kahaba uliyesahauliwa; Piga vizuri, imba nyimbo nyingi, Upate kukumbukwa tena.
Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;