Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Methali 5:4 - Swahili Revised Union Version Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Biblia Habari Njema - BHND lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga, ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. Neno: Bibilia Takatifu lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. Neno: Maandiko Matakatifu lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili. BIBLIA KISWAHILI Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wenye makali kuwili. |
Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.
Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.