Methali 30:19 - Swahili Revised Union Version Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Njia ya tai angani, njia ya nyoka mwambani, njia ya meli baharini, na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke. Biblia Habari Njema - BHND Njia ya tai angani, njia ya nyoka mwambani, njia ya meli baharini, na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza njia ya tai angani, njia ya nyoka mwambani, njia ya meli baharini, na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke. Neno: Bibilia Takatifu Ni mwendo wa tai katika anga, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. Neno: Maandiko Matakatifu Ni mwendo wa tai katika anga, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. BIBLIA KISWAHILI Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana. |
Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe.
bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Maana BWANA asema hivi, Tazama, ataruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Moabu.
Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.
BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;