Methali 3:28 - Swahili Revised Union Version Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo. Biblia Habari Njema - BHND Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo. Neno: Bibilia Takatifu Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. Neno: Maandiko Matakatifu Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. BIBLIA KISWAHILI Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. |
Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiulegeze mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang'anya mali yake; ujira wake aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi.
Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutamani kutenda, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
Lakini niliwatuma hao ndugu, ili kujisifu kwetu kwa ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari, kama nilivyosema;
Waamuru watende mema, wawe matajiri katika kutenda mema, wawe wakarimu na wawe tayari kushiriki na wengine;