Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mathayo 6:26 - Swahili Revised Union Version

Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Waangalieni ndege wa mwituni: Hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Waangalieni ndege wa mwituni: Hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Waangalieni ndege wa mwituni: hawapandi, hawavuni, wala hawana ghala yoyote. Hata hivyo, Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, nyinyi si wa thamani kuliko hao?

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao ndege?

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege?

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mathayo 6:26
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.


Atufundishaye zaidi ya wanyama wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?


Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?


Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.


Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu.


Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.


Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?


Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.