Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.
Mathayo 6:17 - Swahili Revised Union Version Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako, Biblia Habari Njema - BHND Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako, Neno: Bibilia Takatifu Lakini unapofunga, jipake mafuta kichwani na kunawa uso wako, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kunawa nyuso zenu BIBLIA KISWAHILI Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; |
Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa BWANA, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala.
Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unaomboleza, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki;
Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; lakini usijioneshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa.