Mathayo 4:9 - Swahili Revised Union Version akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Biblia Habari Njema - BHND akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.” Neno: Bibilia Takatifu kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote ukinisujudia na kuniabudu.” Neno: Maandiko Matakatifu kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.” BIBLIA KISWAHILI akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia. |
Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwituni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye Juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.
akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
Yesu, huku akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.