Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;
Mathayo 26:57 - Swahili Revised Union Version Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, walikokusanyika waalimu wa sheria na wazee. Biblia Habari Njema - BHND Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, walikokusanyika waalimu wa sheria na wazee. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, walikokusanyika waalimu wa sheria na wazee. Neno: Bibilia Takatifu Wale waliomkamata Isa wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa Torati pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika. Neno: Maandiko Matakatifu Wale waliokuwa wamemkamata Isa wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa Torati pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika. BIBLIA KISWAHILI Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee. |
Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa;
Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lolote;