Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama tini zilizotangulia kuiva; na kikapu cha pili kilikuwa na tini mbovu sana zisizoweza kuliwa, kwa kuwa zilikuwa mbovu sana.
Mathayo 25:2 - Swahili Revised Union Version Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Biblia Habari Njema - BHND Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Neno: Bibilia Takatifu Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Neno: Maandiko Matakatifu Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. BIBLIA KISWAHILI Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. |
Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama tini zilizotangulia kuiva; na kikapu cha pili kilikuwa na tini mbovu sana zisizoweza kuliwa, kwa kuwa zilikuwa mbovu sana.
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.