Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.
Mathayo 24:28 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa popote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. Biblia Habari Njema - BHND Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana popote ulipo mzoga, huko ndiko wakusanyikapo tai. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa popote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. |
Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.
Na wewe, mwanadamu, Bwana MUNGU asema hivi; Sema na ndege wa kila namna, na kila mnyama wa porini, Jikusanyeni, mje; jikusanyeni pande zote mwijie karamu yangu ya kafara ninayoandaa kwa ajili yenu, naam, karamu kuu ya kafara juu ya milima ya Israeli, mpate kula nyama na kunywa damu.
Farasi wao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwamwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitapa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.
Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;