Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa; Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu. Wote wawaonao watatikisa kichwa.
Mathayo 23:31 - Swahili Revised Union Version Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo mnathibitisha nyinyi wenyewe kwamba nyinyi ni watoto wa watu waliowaua manabii. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo mnathibitisha nyinyi wenyewe kwamba nyinyi ni watoto wa watu waliowaua manabii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo mnathibitisha nyinyi wenyewe kwamba nyinyi ni watoto wa watu waliowaua manabii. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. BIBLIA KISWAHILI Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. |
Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa; Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu. Wote wawaonao watatikisa kichwa.
Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake.
na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.
Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulubisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!
Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, nichukuaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;
Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua BWANA, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi.