Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke mahakimu na majaji, watakaowaamua watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; na ukamfundishe yeye asiyezijua.
Mathayo 23:2 - Swahili Revised Union Version Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Waalimu wa sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua sheria ya Mose. Biblia Habari Njema - BHND “Waalimu wa sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua sheria ya Mose. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Waalimu wa sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua sheria ya Mose. Neno: Bibilia Takatifu “Walimu wa Torati na Mafarisayo wameketi kwenye kiti cha Musa, Neno: Maandiko Matakatifu “Walimu wa Torati na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, BIBLIA KISWAHILI Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; |
Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke mahakimu na majaji, watakaowaamua watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; na ukamfundishe yeye asiyezijua.
huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika Sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.
basi, yoyote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,
Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni.
Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako.