Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu.
Mathayo 21:40 - Swahili Revised Union Version Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?” Biblia Habari Njema - BHND “Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Sasa, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyaje hao wakulima?” Neno: Bibilia Takatifu “Basi huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyia nini hao wakulima?” Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa hiyo, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyia nini hao wakulima?” BIBLIA KISWAHILI Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima? |
Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu.
Wakati wa kuvuna matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake.
Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
Basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.
Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?