Mathayo 19:20 - Swahili Revised Union Version Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia; nifanye nini zaidi?” Biblia Habari Njema - BHND Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia; nifanye nini zaidi?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia; nifanye nini zaidi?” Neno: Bibilia Takatifu Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?” Neno: Maandiko Matakatifu Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?” BIBLIA KISWAHILI Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? |
Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wowote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nisherehekee na rafiki zangu;
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.
Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
Nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.
kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.