Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
Mathayo 19:15 - Swahili Revised Union Version Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo. Neno: Bibilia Takatifu Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko. Neno: Maandiko Matakatifu Naye akaweka mikono yake juu yao, na akaondoka huko. BIBLIA KISWAHILI Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko. |
Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.
Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?
Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.