Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 18:5 - Swahili Revised Union Version Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeyote anayempokea mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi. Biblia Habari Njema - BHND Yeyote anayempokea mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeyote anayempokea mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi. Neno: Bibilia Takatifu “Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Neno: Maandiko Matakatifu “Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi. BIBLIA KISWAHILI Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; |
Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Kwa kuwa yeyote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
akawaambia, Yeyote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na yeyote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.
Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimtumaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenituma.
na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu.